RAIS ATTA MILLS WA GHANA AFARIKI DUNIA! - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Wednesday, July 25, 2012

RAIS ATTA MILLS WA GHANA AFARIKI DUNIA!

 

Hayati Atta Mills.
 



Accra-GHANA,
Rais Atta Miils wa Ghana amefariki dunia ghafla siku ya Jumanne imearifiwa, Rais Mills ambaye alijizolea sifa kubwa barani Afrika na Duniani kwa ujumla kwa kuboresha na kusimamia demokrasi ndani na nje ya mipaka ya nchi yake amearifiwa kufariki ghafla akiwa na umri wa miaka 68.

Rais huyo amefariki siku chache baada ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa hapo jumamosi iliyopita . Sababu za kifo chake  bado hazijawekwa wazi.ingawa mmoja wa ndugu wa karibu ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema rais huyo alikuwa akilalamika kuwa anajisikia maumivu tangu siku ya Jumatatu jioni na kufika siku ya jumanne mauti yalimfika.

Msemaji wa ofisi ya rais alitangaza kifo hicho, ambapokwa kufuata katiba ya nchi hiyo, makamu wa rais wa nchi hiyo bw. John Dramani Mahama (53) aliapishwa kuwa rais wa muda,saa chache baada ya kutangazwa kwa kifo hicho.

Rais huyo amefariki miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ambapo alitarajiwa kutetea kiti chake hicho mnamo mwezi Desemba mwaka huu.Atakumbukwa kwa kusimamia demokrasi ya kweli katika taifa hilo kinara wa kuzalisha dhahabu Afrika na mzalishaji namba mbili wa Cocoa duniani.

No comments: