Taarifa zinasema kuwa aliyekuwa mchezaji na kocha msaidizi wa Manchester United Ryan Giggs ameonekana kuwa tayari kuifundisha Swansea City ikiwa Francesco Guidolin atachukuwa sehemu ya umiliki wa klabu hiyo.
Giggs, 42, aliiacha nafasi yake kama meneja msaidizi wa Manchester United tangu Julai na sasa yupo huru akifanya shughuli zake binafsi.
Swansea wamechukua pointi nne kutoka mechi tano msimu huu na wameripotiwa kuwa na mpango wa kubadili kocha.
Taarifa zimeongeza kuwa kama kutatokea mabadiliko hayo basi Giggs ni chaguo pekee kwa klabu hiyo.
Tangu kuondoka Old Trafford katika majira ya joto, Giggs amekuwa na muda mrefu akijidhughulisha na shughuli za kibiashara, na kazi za uchambuzi katika TV.
Giggs amemaliza mafunzo na kupata beji ya ukocha na ameonesha shauku ya kuwa kocha na hasa Swansea.
No comments:
Post a Comment