Imetimia miaka 36 sasa tangu mfalme wa muziki wa reggae duniani, Robert Nesta Marley Maarufu kwa jina la ‘Bob Marley’ tangu afariki dunia Mei 11,1981 huko Miami nchini Marekani.
Aidha, Bob alifariki akiwa na miaka 36 na leo ametimiza miaka 36 tangu kifo chake. Bob Marley alizaliwa Februari 6 mwaka 1945 katika kijiji cha nine Mile huko Saint Ann Parish nchini Jamaica na mama yake mweusi, Cadella Booker huku baba yake mzazi akiwa ni Mzungu ambaye alijulikana kwa jiana la Norvall Marley.
Hata hivyo, Bob alipata heshima kubwa kwenye muziki wa reggae kutokana na nyimbo zake kuzungumzia maisha halisi na kuhubiri amani baina ya watu wa mataifa na rangi tofauti huku akikemea vitendo vinavyokiuka haki za binadamu
No comments:
Post a Comment