MDEE,NASARI WAKANUSHA KUMPIGIA DEBE ZITTO URAIS 2015. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Wednesday, July 25, 2012

MDEE,NASARI WAKANUSHA KUMPIGIA DEBE ZITTO URAIS 2015.

 



Dar Es Salaam- TANZANIA,
Baada ya siku chache kudaiwa na vyombo vya habari kuwa wanamnadi mbunge wa Kigoma kaskazini Mh. Zitto Kabwe kuwania urasi mwaka 2015,Wabunge wawili wa Chadema Mh.Joshua Nasari na Halima Mdee, wamejitokeza na kukanusha taarifa hizo.

Kwa Upande wake Nassari hapo jana ametoa taarifa kwa vyombo mbali mbali vya habari akikanusha taarifa hizo na kudai kuwa ni uzushi na kwa upande wake hajawahi kusimama na kutamka maneno hayo.

Nasari alisema anaamini vitu muhimu ni mizizi au vyanzo vya matatizo yanayowakabili Watanzania kama umaskini, ujinga, maradhi, ufisadi na utawala mbovu wa Chama Cha Mapinduzi CCM na sio yo urais.

“Kama ambavyo chama changu, Watanzania wengine makini na mimi mwenyewe, naamini kuwa kwa sasa suala la muhimu kwetu kama Taifa ni kutafuta mizizi au vyanzo vya matatizo mbalimbali yanayoikabili jamii ya Watanzania,” alinukuliwa Nasari..


Kwa upande wake Mbunge wa Kawe Mh.Halima Mdee naye pia ametoa taarifa ya kukanusha habari hiyo akisema kimevunja misingi ya maadili ya vyombo vya habari kwa Uzushi huo.

“Habari hiyo imeniletea usumbufu mkubwa hasa kwa wananchama wa chama changu cha Chadema ambao wanajua kuwa chama chao makini ni mahiri katika kufuata katiba, kanuni na taratibu katika kuendesha mambo yake kwa manufaa ya watu wote,” alinukuliwa Mdee.
 
Gazeti hilo lilidaiwa kumnukuu Nasari wakati alipofika Kigoma ambapo liloidai alitamka kuwa Zitto anafaa kuwa ndiye rais ajaye wa Tanzania


No comments: