Timu ya Real Madrid ya Hispania leo hii imeusogelea ubingwa baada ya kuifunga timu ya Celta vigo kwa magoli 4-1, magoli ya Madrid yamefungwa na Ronaldo(dk 10&48),Benzema dk 70 na Kroos dk.88, huku goli la kufutia machozi la Celta vigo likifungwa dk.69 na Guidetti.
Katika Mchezo huo Celta vigo walilazimika kumaliza wakiwa pungufu baada ya mchezaji wa Iago Aspas kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kupewa kadi mbili za njano.
Kwa matokeo hayo Madrid wamefikisha pointi 90 wakiwazidi mhasimu wao Barcelona kwa pointi 3 huku wakiwa wamelingana michezo na watahitaji kushinda mchezo wao wa mwisho wa ligi dhidi ya Malaga siku ya jumapili ili kuwa mabingwa wapya wa ligi ya Uhispania.
MSIAMO WA LIGI YA UHISPANIA BAADA YA MCHEZO WA LEO:
No comments:
Post a Comment