WATU 12 WAUAWA KWA RISASI KATIKA UKUMBI WA SINEMA MAREKANI - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Friday, July 20, 2012

WATU 12 WAUAWA KWA RISASI KATIKA UKUMBI WA SINEMA MAREKANI

http://l.yimg.com/bt/api/res/1.2/znL0A21JQtRoQoGuGkbIXA--/YXBwaWQ9eW5ld3M7Y2g9NDA3O2NyPTE7Y3c9NjMwO2R4PTA7ZHk9MDtmaT11bGNyb3A7aD00MDc7cT04NTt3PTYzMA--/http://l.yimg.com/os/152/2012/07/20/colorad-jpg_141900.jpg
Baadhi ya ndugu na Jamaa wa Marehemu na Majeruhi katika eneo la tukio

 Denver,Colorado MAREKANI,
Kijana wa Umri mwenye umri wa miaka 24 aliyetambulika kwa jina la James holmes  akivalia kificha uso amewashambulia na kuwauwa kwa risasi watu 12 na kujeruhi wengine zaidi ya 50 katika ukumbi wa sinema wa Century Aurora 16 r katika kitongoji cha Denver-Colorado huko Marekani usiku wa kuamkia Ijumaa ya leo. 

Watu hao walikuwa katika ukumbi huo wa sinema wakiangalia filamu mpya ya Batman inayofahamika kama  "The Dark Knight Rises" .Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa muuaji aliingia ndani ya ukumbi na kutupa mabomu ya machozi na kisha kuanza kurusha risasi akiwalenga watazamaji.

Polisi mjini Colorado wamemkamata mtuhumiwa huyo ambaye ametambulika kwa jina la James Holmes ambaye aliwapigia polisi na kuwaambia kuwa alikuwa na vitu vyenye milipuko huko nyumbani kwao.

  
 Watu kumi na mbili wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya hamsini wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Rais Obama ametoa salaam za rambi rambi kwa familia za ndugu na jamaa wa familia zilizokumbwa na janga hilo na kuwataka wawe pamoja kama familia moja ya Kimarekani.Rais obama pia amesema atafanya kila awezalo kuhakikisha muuaji anafikishwa katika vyombo vya dola.

No comments: