YANGA SC imerudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutokana na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City ya Mbeya jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ushindi huo unawafanya mabingwa hao watetezi watimize pointi 65 baada ya kucheza mechi 28 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu. Simba inaangukia nafasi ya pili kwa pointi zake 65 za mechi 29, ikizidiwa wastani wa mabao.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Andrew Shamba wa Pwani, aliyesaidiwa na Joseph Pombe wa Shinyanga na Haji Mwalukuta wa Tanga, dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika Yanga ikiwa inaongoza 1-0.
No comments:
Post a Comment