RUSSIA NA CHINA WAKWAMISHA ADHIMIO LA UN DHIDI YA SYRIA KWA VETO. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Thursday, July 19, 2012

RUSSIA NA CHINA WAKWAMISHA ADHIMIO LA UN DHIDI YA SYRIA KWA VETO.

Russia na China wamepiga kura za Veto leo hii  katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa kupinga hatua kali dhidi ya Syria na kukwamisha juhudi za kumaliza vurugu nchini humo.kura hizo zimekwamisha juhudi ya nchi za Mashariki za kutaka hatua kali dhidi ya Syria.
 Hiyo ni mara ya tatu kwa nchi hizo kupiga kura hizo ambapo nchi hizo mbili zimekuwa zikipinga hatua kali dhidi ya serikali ya Syria ambayo imekuwa chanzo cha vurugu na mauaji ya maelfu yaliyodumu kwa miezi 16.

Katika kura hizo ambazo azimio lake lingeongeza muda wa waangalizi wa umoja wa kimataifa nchini Syria nchi 11 zililiunga mkono, nchi mbili hazikupiga kura ambazo ni Afrika kusini na Pakistan, na nchi mbili zililipinga ambazo ni china na Russia.

Akiongea kwa masikitiko msimamizi wa umoja wa mataifa katika suluhu ya Umoja wa mataifa Bw. Koffi Annan amesema baraza limeshindwa kuchukua maazuzi imara na muhimu aliyoyategemea katika kumaliza vurugu na mauaji nchini Syria.

Waasi wazidi kusogea karibu na ngome ya serikali:
Wakati juhudi za kidiplomasia zikishindikana  wassi wamezidi kusogea katika ngome ya serikali baada ya hapo jana juzi kuwauwa viongozi muhimu katika serikali ya Syria.

No comments: