RAIS MPYA WA INDIA ATANGAZWA-ni Pranab Mukherjee - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Sunday, July 22, 2012

RAIS MPYA WA INDIA ATANGAZWA-ni Pranab Mukherjee




INDIA,
 Aliyewahikuwa waziri wa fedha wa zamani wa India Bw.Pranab Mukherjee amechaguliwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo kwa kushinda zaidi ya nusu ya kura zilizopigwa na mabunge ya nchi hiyo. Kwa kawaida uchaguzi wa rais nchini India hufanywa na mabunge mawili na rais huwa hana madaraka makubwa kama ilivyo kwa nchi za kijamhuri kama Tanzania.

Mukherjee, 76, mfuasi wa chama cha Congress alikuwa akitumainiwa kushinda kiti hicho kutokana na kukubaliwa na watu wengi wakiwemo wale wa kutoka vyama pinzani tofauti na mpinzani wake Bw.Pumo A. Sangma (64) aliyewahi kuwa spika wa bunge la nchi hiyo anayetoka katika chama cha Bharatiya Janata Party.

 Licha ya kile kilichoonekana imani katika matamshi yake ya mwezi uliopita kuwa nafasi hiyo inatakiwa kutolewa tu na sio kufikiriwa au kuhangaikiwa Bw. Mukherjee amefanya juhudi za ziada kupata nafasi hiyo hasa alipokuwa akitaka uungwaji mkono na wa vyama vya upinzani vyenye mlengo wa kushoto.

Rais wa India huchaguliwa na wabunge 4'896 kutoka majimbo mbali mbali nchini humo na ushindi huo wa Mukherjee utaongeza nguvu ya serikali bungeni, wakati ambao inalaumiwa kwa ukuaji mdogo wa uchumi na tuhuma mbali mbali za utumiaji mbov wa ofisi za umma.

No comments: