OLYMPIC KUFUNGULIWA LEO-Picha za Maandalizi ya Mwisho. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Friday, July 27, 2012

OLYMPIC KUFUNGULIWA LEO-Picha za Maandalizi ya Mwisho.

http://london-games.reuters.com/london-olympics-2012/files/styles/article_large_landscape/public/photo_item/OLYMPICS-BRITAIN/0/2012-05-05T212906Z_922909035_GM1E8560FH101_RTRMADP_3_OLYMPICS-BRITAIN.JPG
Uwanja wa Olympic ukiwa tayari kwa sherehe za ufunguzi.

 Kengele zimelia usiku wa kuamkia leo nchini uingereza kuashiria Siku ya mwisho kabisa kuelekea ufunguzi wa mashindano ya Olympic utakaofanyika leo usiku ndani ya uwanja wa Olympic park katika jiji la London na kuhudhuriwa na watu maarufu wakiwemo Malkia Elizabeth na Michelle Obama mke wa Rais wa Marekani.
http://london-games.reuters.com/london-olympics-2012/files/styles/article_large_landscape/public/photo_item/SPORTS-US-OLY-BLUNDERS-ADV1/2/2012-07-26T201622Z_1_CBRE86P1KBF00_RTROPTP_3_SPORTS-US-OLY-BLUNDERS-ADV1.JPG
Taa ndani ya uwanja zikiwa tayari kwa sherehe hizo.

Sherehe hizo zinatakazokuwa na shamra mbali mbali zikiwemo ulipuaji wa mafataki, muziki, na maonesho mbalimbali ya kimichezo na kitamaduni zinatarajiwa kufana na kuvutia wahudhuriaji zaidi ya 60,000 na watazamaji zaidi ya bilioni 1 dunia nzima.

http://london-games.reuters.com/london-olympics-2012/files/styles/article_large_landscape/public/photo_item/OLYMPICS-OPENING/0/2012-06-12T113443Z_1830676218_LM1E86C0W2F01_RTRMADP_3_OLYMPICS-OPENING.JPG
Muundo wa uwanja wa lympic utakavyokuwa katika sherehe hizo.

http://london-games.reuters.com/london-olympics-2012/files/styles/article_large_landscape/public/photo_item/OLY-AROUNDTOWN-ADV1/0/2012-07-26T205633Z_10312663_GM1E87R0DMU01_RTRMADP_3_OLY-AROUNDTOWN-ADV1.JPG
Jua likipenya kati ya bendera ya nchi zinazoshiriki mashindano hayo katika viwanja vya Bunge la Uingereza.



Mwenge wa olympic leo umemaliza ziara yake kwa kurudi london ambapo ulipitia mto Thames ndani ya majahazi ya kifalme ya Gloriana ambayo yalitumika pia katika sherehe za  Malkia Elizabeth mwezi juni.

http://london-games.reuters.com/london-olympics-2012/files/styles/article_large_landscape/public/user_upload/14541/2/RTR35DVV.jpg
Mkimbiza mwenge Amber Charles akiwa amebeba mwenge kutoka katika jahazi la kifalme chini ya daraja la 'Tower' Lonndon leo hii.

Viwanja vimeonekana kuwa tayari na watu wote wanahamasa jijini London juu ya kuanza kwa michezo hiyo ambayo imeigharimu nchi ya Uingereza zaidi ya trilioni 21 katika maandalizi yake.

            Kila la kheri kwa waingereza na wanamichezo wote wenye ushiriki katika michezo hiyo!

No comments: