MWENGE WA OLYMPIC WAWASILI LONDON. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Saturday, July 21, 2012

MWENGE WA OLYMPIC WAWASILI LONDON.

Ndege iliyobeba Mwenge wa Olympic ikiwasili mjini London Hapo Jana (REUTERS)

 LONDON-UINGEREZA,
Mwenge wa Olympic Umewasili mjini London jana  kuanza ziara yake ya mwisho  kabisa katika mji wa  ikiwa imebaki wiki moja kabla ya michezo ya Olympic kuanza.

 Mwenge huo uliwasili kwa kutumia Helkopta maalum ya kijeshi na kushushwa na Kamanda wa kikosi cha Maji ambaye alishuka kutoka juu ya Helkopta kwa kutumia kamba maalum na kutua katika mnara wa London ambao ni moja ya vivutio maarufu vya utalii Jijini humo.

http://l3.yimg.com/bt/api/res/1.2/KpMpumtXf1pwZXNwjsA0bg--/YXBwaWQ9eW5ld3M7Zmk9aW5zZXQ7aD00MDY7cT04NTt3PTYzMA--/http://media.zenfs.com/en_us/News/ap_webfeeds/58637e46559eeb14150f6a706700222e.jpg
Kamanda wa kijeshi akishuka na Mwenge wa Olympic(REUTERS)
Baada ya hapo mwenge huo unatarajiwa kutembelea maeneo muhimu ya kidini,kisiasa na kifalme katika jiji hilo. Michezo ya Olympic inaanza rasmi tarehe 27 julai mpaka Agosti 12 2012, ambapo kwa sasa imebaki takribani chini ya wiki moja tu kuanza kwa michezo hiyo. Maafisa wa Uingereza wanaamini michezo hiyo itakuwa na mafanikio licha ya matishio kadhaa likiwemo la mvua na migomo kwa wafanyakazi hasa wa vyombo vya usafiri.

 

No comments: