Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hans Poppe ameachia ngazi.
Habari za uhakika zimeeleza kuwa Hans Poppe ameandika barua ya kuachia ngazi akiona mambo yanaendeshwa ndivyo sivyo.
“Hans Poppe ameachia ngazi kwa kuwa hakufurahishwa na mlolongo ulivyokuwa hadi Simba kuingia mkataba wa SportPesa,” kilieleza chanzo.
"Hans Poppe ameandika barua kujiuzulu kwenye kamati ya utendaji, maana yake anaondoka automatically katika nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya usajili.
"Kilichomchukiza, kuna kundi lililoongozwa na Rais Evans Aveva na makamu Geofrey Nyange Kaburu, lilifanya mambo kimya kimya na Hans Poppe amesema hana Mo Dewji aliyeisaidia Simba mishahara naye hakushirikishwa hata kiungwana tu, hivyo amepinga hilo."
No comments:
Post a Comment