CHELSEA MABINGWA EPL! - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Saturday, May 13, 2017

CHELSEA MABINGWA EPL!



Wachezaji wa Chelsea baada ya mchezo

mfungaji wa goli la ushindi Michy Batshuayi
Mashabiki wa Chelsea wakishangilia na mano wa kombe

Goli la pekee lilifungwa na mchezaji ambaye hajapewa nafasi kubwa katika msimu huu katika kikosi cha Chelsea  Michy Batshuayi katika dakika ya 82 limetosha kuipa ubingwa wa ligi kuu maarufu kama EPL timu hiyo.

Chelsea wakicheza ugenini  ambapo walikaribishwa na West brom wamechukua ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kupata ushindi wa 0-1 .


Tottenham ambao walikuwa  wapinzani wa karibu wa Chelsea katika nafasi ya pili, walipoteza mchezo wao dhidi ya West Ham Mei 5, na hivyo kuifanya Chelsea kuhitaji kushinda mechi mbili kati ya nne zilizosalia.

Walishinda mechi yao dhidi ya Middlesbrough 3-0 Jumatatu Mei 8, na kukamilisha pointi walizohitaji kuchukua ubingwa kwa kuizaba West Brom siku ya Ijumaa Mei 12.

No comments: