Serikali ya Marekani imeidhinisha dola milioni 526 katika kipindi cha
mwaka mmoja ujao kwa ajili ya kukabiliana na VVU na Ukimwi Tanzania.
Msaada huu kupitia mpango wa dharura wa Rais wa nchi hiyo wa
kukabiliana na ukimwi (PEPFAR) utaongeza idadi ya Watanzania wanaopatiwa
matibabu ya kufubaza VVU kufikia milioni 1.2.
Aidha utaimarisha mapambano dhidi ya VVU kupitia huduma za upimaji,
matibabu, kufubaza na kuzuia maambukizi ili hatimaye kufikia lengo la
kutokomeza ukimwi ifikapo mwaka 2030.
Taarifa ya ubalozi wa Marekani nchini imesema fedha hizo zitafadhili
miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa utekelezaji wa PEPFAR
utakaoanza kutekelezwa Oktoba hadi Septemba 2018, na ni ongezeko la
asilimia 12.3 ya bajeti ya mwaka jana.
Bajeti iliyotengwa inajumuisha pia utoaji wa huduma na matibabu kwa
watoto yatima na walio katika mazingira hatarishi pamoja na kukabiliana
na ukatili wa kijinsia.
PEPFAR pia itasaidia mpango wa tohara ya hiari kwa wanaume, walengwa wakiwa 890,000.
Mpango huu unaendeleza ubia wa muda mrefu kati ya Marekani na
Tanzania katika sekta ya afya ikiwa ni pamoja na muongo mmoja wa
ushirikiano uliowezesha kudhibiti kwa mafanikio maambukizi ya VVU.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser alisema, “Kwa pamoja
tunafanya kazi ili hatimaye kuwa na kizazi kisicho na Ukimwi Tanzania –
ambacho hakuna hata mtu mmoja anayeachwa nyuma.
CHANZO:VOA
No comments:
Post a Comment