Simba SC imerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stand United ya Shinyanga jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wekundu wa Msimbazi wanafikisha pointi 65 baada ya ushindi wa leo wakiwa wamecheza mechi 29, mbili zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye pointi 62, ambao wanaweza kurudi kileleni kwa mabao zaidi, wakiifunga Mbeya City kesho Uwanja wa Taifa.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua, Stand United ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa nyota wake, Suleiman Kassim ‘Selembe’ aliyefunga sekunde ya 58 dakika ya kwanza.
No comments:
Post a Comment