Serengeti Boys imeandika ushindi wa
kwanza wa michuano ya Afcon chini na taratibu ni dalili za kuingia hatua
ya nusu fainali ambayo ni tiketi ya kucheza Kombe la Dunia.
Serengeti imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Angola na kupata pointi nne.
Mechi ya kwanza, Serengeti ilianza kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Mali ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo.
Katika mchezo wa leo, Serengeti Boys
ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 6 tu kupitia kwa Kelvin
Naftali aliyeunganisha krosi safi ya Yohana Mkomola.
Angola awalijitutumua na kusawazisha
katika dakika ya 18 kupitia kwa Pedro Augustino lakini Serengeti
wakakomaa nao na kufunga bao la pili katika dakika ya 69 kwa bao la
Abdul Selemani.
No comments:
Post a Comment