Manchester City wamepata ushindi muhimu hapo jana unaowapeleka nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi ya EPL, ushindi huo dhidi ya West bromwich Albion umeifanya Manchester City kufikisha pointi 75 ikibakiwa na mchezo mmoja mkononi kumaliza ligi.
Magoli ya Jesus (dak 27), debrune (dak 29), Y'Toure (dk.57) yaliifanya Manchester city kuibuka na ushindi wa magoli 3-1,huku goli la west bromwich likifungwa na Robson dak.87.
Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo Arsnal iliifunga Sunderland kwa magoli 2-0, magoli yote yakifungwa na Sanchez dak.72 na 81, hivyo kufikisha pointi 72 ikiwa imebakiza mchezo mmoja mkononi dhidi ya everton, hivyo itatakiwa kushinda mchezo huo na kuombea Liverpool ipoteze mchezo wake wa mwisho middlesbrough.
kwa matokeo hayo hii ndiyo nafasi ya timu nyingine katika kinyang'anyiro cha nafasi nne za juu;
No comments:
Post a Comment