HUYU NDIYE MTU MPYA ALIYECHAGULIWA KUMCHUNGUZA TRUMP NA URUSI. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Thursday, May 18, 2017

HUYU NDIYE MTU MPYA ALIYECHAGULIWA KUMCHUNGUZA TRUMP NA URUSI.


Wizara ya sheria nchini Marekani, imetangaza kuteuliwa kwa mwendesha mashtaka maalum atakae ongoza uchuguzi wa tuhuma kwamba Urusi iliingilia uchaguzi wa marekani wa mwaka jana. 

Mwendesha mashtaka huyo aliwahi kuwa mkuu wa shirika la kijajusi la FBI, Robert Mueller. 

Pia katika uchunguzi wake, atazingatia iwapo kulikuwa na mwingiliano wa aina yoyote kati ya Urusi na timu ya kampeni ya Trump.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya sheria nchini humo imesema uchunguzi huo utaongozwa na mtu asiyeegemea upande wowote kwa ajili ya maslahi ya umma.

Tangazo hilo linafuatia utata uliogubikwa kufuatia kufutwa kazi kwa wiki moja iliyopita kwa James Comey, ambae ndie aliyekuwa akiongoza uchunguzi huo.

No comments: