CIA YAIVALIA NYUGA KOREA KASKAZINI, HAYA NDIYO MAAMUZI MAPYA. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Friday, May 12, 2017

CIA YAIVALIA NYUGA KOREA KASKAZINI, HAYA NDIYO MAAMUZI MAPYA.


Shirika la CIA la Marekani  limeanzisha kitengo  maamum kushughulikia Korea kaskazini na vitisho vyake vya Nyuklia.Shirika hilo  limetoa taarifa siku ya jumatano kuwa linaanzisha kituo hicho ili kujidhatiti na tabia zisizoeleweka za Kiongozi wa korea Kaskazini Kim Jong Un na taifa lake.

"Kuundwa kwa kituo hicho kutasaidia kuunganishwa na kutumika ipasavyo kwa rasilimali, uwezo na mamlaka katika kupambana na Vitisho vya Korea Kaskazini' ilisema taarifa ya CIA.

Kituo hicho kilichowekwa makao makuu ya CIA huko Langley, Virginia, kitakusanya wachambuzi na maafisa wa CIA ambao watafanya kazi pamoja kuichambua na kuunda mbinu dhidi ya Korea Kaskazini.

"Kituo hiki kitawatumia maafisa wenye uzoefu kutoka CIA ambao wataunganisha utaalamu wao na ubunifu dhidi ya lengo la korea Kaskazini" aliongeza Heather Fritz Horniak msemaji wa CIA.

Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa katika taharuki wakati ambao Korea Kaskazini inatishia kuishambulia Marekani na wiki hii ikionekana kutaka kufanya jaribio jingine la Nyuklia, huku Marekani nayo ikionekana kujiandaa na tishio hilo kwa kufanya mazoezi ya kijeshi Huko Korea Kusini.

No comments: