Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzaniabara, leo November 2 2016 walishuka katika uwanja wa Sokoine Mbeya kucheza dhidi ya wenyeji wao Mbeya City katika mchezo wao wa 13 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017.
Yanga wakiwa ugenini huku wakiwa na kumbukumbu ya kipigo chao cha kwanza kutoka Stand United cha goli 1-0 September 25 2016, leo November 2 2016 wamekubali kipigo cha pili kutoka kwa Mbeya City wakiwa katika dimba la Sokoine Mbeya.
Mbeya City wamefanikiwa kuifunga Yanga goli 2-1, magoli ambayo yalifungwa na Mwasapilidakika ya 6 na Kenny dakika 36 goli ambalo lilichukua muda kidogo refa kufanya maamuzi kutokana na wachezaji wa Yanga kuligomea,Donald Ngoma ndio alifunga goli la kufutia machozi la Yanga dakika 4 za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko.
Wednesday, November 2, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment