Kuu soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017 umeendelea kwa michezo sita kupigwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, wakati Mabingwa watetezi Yanga wakiwaMbeya kucheza dhidi ya Mbeya City, watani zao Simba walikuwa Shinyanga kuwakabiliStand United.
Simba wakiwa katika uwanja wa ugenini wenye rekodi nzuri kwa wenyeji Stand Unitedkutokupoteza mchezo katika uwanja huo kwa msimu huu, wamekuwa timu ya kwanza kuondoka na point tatu dhidi ya Stand Unitedkatika uwanja wa Kambarage.
Katika mchezo huo ambao Simba walikuwa na tahadhari kutokana na Stand Unitedkuwafunga Yanga na Azam FC katika uwanja huo, Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Shiza Kichuya kwa mkwaju wa penati dakika ya 33 baada ya Laudit Mavugo kufanyiwa faulo katika eneo la hatari.
Wednesday, November 2, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment