Manchester City jana wamelipa kisasi kwa Barcelona baada ya ushindi wa magoli 3-1 katika uwanja wao wa nyumbani.
Barcelona ndiyo waliokuwa wa kwanza kufunga kwa goli la Lionel Messi dk.21ambapo lilikuwa pia goli lake la 90 katika UEFA champions League.
Man City walianza mashambulizi ya kushitukiza na kufanikiwa kupata goli la kusawazisha dakika ya 39 kupitia kwa Gundogan aliyetengenezewa na Stelling.
Kevin De Bruyne alifnga goli la pili kwa Man city baada ya kupiga faulo nzuri iliyomshinda kipa wa Barca na kuingia golini moja kwa moja.
Gundogan alifunga goli la tatu na la ushindi baada ya mpira krosi ya De Brune kushindwa kuokolewa na mabeki wa Barca.
Kwa upande mwingine Arsenal awliokuwa ugenini jana wameshinda 3-2 baada ya vuta nikuvute dhidi ya Ludo Razgd.
MATOKEO KWA UJUMLA:
No comments:
Post a Comment