Meneja wa Manchester City Pep
Guardiola, anasema kuwa mechi kati ya klabu yake na Barcelona inastahili
kuchukuliwa ni kama fainali.
Manchester City ilichapwa mabao 4-0
na Barcelona kwenye mechi ya kundi C iliyochezwa nchini Uhispania
kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya.Sergio Aguero anatarajiwa kuwa katika kikosi cha kwanza cha Manchester City naye Pablo Zabaleta akiwa katika upande wa ulinzi.
"Tulipoteza pointi mbili dhidi ya Celtic kwa hivyo tunahitaji pointi hizo," alisema Guardiola ambaye ni meneja wa zamani wa Barcelona.
"Si fainali kwao, lakini ni fainali kwetu," aliongeza Guardiola.
Hata hivyo kikosi cha Barcelona hakitakuwa na nahodha Andres Iniesta ambaye ana jeraha pamoja na walinzi Gerard Pique, Jordi Alba, Aleix Vidal na Jeremy Mathieu, ambao wote walitimuliwa wakati wa mechi ya kwanza.
Kwa upande wake meneja wa Barcelona Luis Enrique, amesema kuwa mambo yatawakuwa ni yale yale yaliyoshuudiwa kwenye uwanja wa Camp Nou.
MECHI NYINGINE:
No comments:
Post a Comment