RAIS MAGUFULI AFANYA UZINDUZI KENYA - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Tuesday, November 1, 2016

RAIS MAGUFULI AFANYA UZINDUZI KENYA


Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta leo wamezindua barabara ya Southern By-pass iliyojengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi nchini Kenya.

Sherehe ya uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 28 na inayounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi imefanyika katika eneo la Karen nje kidogo ya Jiji la Nairobi.

Akizungumza katika sherehe hiyo Rais Magufuli amempongeza Rais Kenyatta na Serikali yake kwa kujenga barabara hiyo ambayo sio tu itawasaidia wananchi wa Kenya bali pia itawasaidia wananchi wa Afrika Mashariki wanaotumia barabara zinazopitia Nairobi.

No comments: