Bingwa wa masumbwi wa dunia mstaafu, Floyd Mayweather amekuwa mwanamichezo maarufu wa kwanza kukutana na rais mteule wa Marekani, Donald Trump tangu aliposhinda uchaguzi wa urais.
Mayweather ambaye alikuwa jijini New York akipigia debe pambano la masumbwi kati ya Badou Jack na Brit Degale, alifika katika ofisi za bilionea huyo zinazojulikana kama ‘Trump Tower’ na kupiga picha ya pamoja.
Katika picha hiyo pia anaonekana mtoto wa kiume wa Trump, Donald Jr ambaye baadae aliipost kwenye mitandao ya kijamii.
Trump amekuwa shabiki wa Mayweather kwa muda mrefu na alihudhuria pambapo kati ya bondia huyo na Manny Pacquiao lililofanyika mwaka jana. Mayweather alishinda pambano hilo na baadae akatangaza kustaafu baada ya pambano moja la ziada. Alistaafu na kuweka rekodi ya kutoshindwa pambano hata moja.
No comments:
Post a Comment