Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ametia saini Sheria ya huduma za Habari nchini ya mwaka 2016 iliyopitishwa bungeni na Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wake wa 5 mjini Dodoma.
Taarifa hiyo iliyotolewa leo Novemba 17, 2016 na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa imeeleza kuwa Rais Magufuli amesaini Sheria hiyo Novemba 16, 2017 na amewapongeza wadau wote waliofanikisha kutungwa kwa Sheria hiyo.
Amesema Rais Magufuli amesema anaamini Sheria hiyo itasaidia kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma wenyewe na Taifa.
No comments:
Post a Comment