URUSI YAFANYA MAAMUZI YA SILAHA DHIDI YA MAREKANI - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Tuesday, October 4, 2016

URUSI YAFANYA MAAMUZI YA SILAHA DHIDI YA MAREKANI

Russia imesimamisha mkataba wa kuharibu  silaha za plutonium iliyoingia na Marekani, ishara ya karibuni ya hali mbaya ya mahusiano baina ya nchi.Akitangaza hilo Rais Vladimir Putin ameituhumu Marekani kujenga tishio la makubaliano hayo kutokana na vitendo vyake vya kichokozi kwa Urussi.

Katika taarifa hiyo serikali hiyo ya Moscow imeweka masharti ya kurudishwa kwa mkataba huo.Moscow pia kuweka kabla ya masharti ya Marekani kwa mpango wa kuwa na tena.
Chini ya makubaliano hayo kila nchi ilitakiwa kuharibu tani 68 za plutonium ambayo ilikuwa na uwezo wa kutengeneza silaha 17,000 za Nyuklia.



Marekani hapo awali nayo ilitangaza kusimamisha mazungumzo na Urusi kuhusu Syria ikiituhumu serikali ya Urusi kukiuka makubaliano ya mkataba wao.

Kuvunjwa kwa mikataba hiyo ni tishio kuwa huenda mbeleni nchi hizo zikaingia katika mgogoro mkubwa zaidi unaoweza kupelekea matumiziya silaha.

Mahusiano ya Marekani na Urusi yameharibika zaidi mwezi uliopita tangua Urusi ilipoanza kampeni yake ya kupiga mabomu huko Syria.


No comments: