KABILA AZINDUA JENGO TPA, UFARANSA YAMPIGA MKWARA - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Tuesday, October 4, 2016

KABILA AZINDUA JENGO TPA, UFARANSA YAMPIGA MKWARA

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Bw.Joiseph Kabila amezindua jengo la One Stop Centre amabalo litatoa huduma za forodha kwa mizigo inayoingia na kutoka katika bandari ya Dar Es Salaam.

Rais Kabila amesema anarudhishwa na utendaji wa bandari ya Dar es salaam na kuiomba serikali ya Tanzania kuboresha miundombinu hasa ya barabara, reli na anga ili kuimarisha mahusiano ya kibiashara kati ya Congo na Tanzania.

Wakati huo huo Ufaransa imesema Rais Joseph Kabila ni sharti aheshimu katiba na kujiuzulu mwishoni mwa muhula wake ,waziri wa maswala ya kigeni nchini Ufaransa Jean-Mark Ayrault amesema katika mahojiano na kituo cha habari cha TV5.

Bwana Ayrault alikuwa akisisitiza wito aliotoa wiki iliopita wakati akiwahutubia wanafunzi mjini Paris.

Wakati huu aliangazia madai kwamba Ufaransa imekuwa ikiingilia maswala ya ndani ya DRC,akisema kuwa taifa lake haliko pekee kumkumbusha Kabila kwamba lazima aheshimu sheria.

Aliambia kituo hicho: ''Rais Kabila lazima aonyeshe mfano mwema. Ni lazima aheshimu katiba. Iwapo vikwazo vitahitajika tutaamua kuvitekeleza. Nataka watu waelewe; Watu waliopo katika mamlaka DRC ni lazima wawajibike. Iwapo wanahitaji amani nchini mwao, iwapo wanajali hali ya watu wao ,ni lazima wafuate katiba''.

No comments: