Shirikisho
la Soka nchini TFF limesema hivi sasa wanaangalia zaidi maendeleo ya
timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania Serengeti Boys na siyo kuvutana juu
ya mchezaji wa timu ya taifa ya vijana ya Congo Brazzaville.
Katibu
Mkuu wa TFF Mwesigwa Celestine amesema, suala la mchezaji huyo
wameliacha chini ya Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF ambapo
wameagiza mchezaji huyo kufanyiwa upya vipimo ambavyo hapo awali Namibia
walishindwa kutokana na gharama ambazo walitakiwa kuzilipia wao
wenyewe.
Mwesigwa
amesema, mchezaji huyo anadaiwa kuwa na umri zaidi ya ule unaotakiwa na
alivaa namba 05 katika mchezo wa timu ya Taifa ya Namibia dhidi ya Timu
yake ya Congo Brazzaville na katika mchezo dhidi ya Serengeti Boys
alivaa jezi namba 10 huku katika mchezo wa mwisho ambao Congo
walifanikiwa kufuzu kuelekea katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa
kuichapa Serengeti Boys bao 1-0 alivalia jezi namba 10.
Wednesday, October 5, 2016
New
HAYA NDIYO MAAMUZI YA TFF JUU YA KIJEBA WA CONGO ALIYESHIRIKI KUITOA SERENGETI
HABARI ZA KITAIFA NA KIMATAIFA
habarimpya,
michezo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment