October 17
2016 iliripotiwa taarifa iliyomhusu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya
ya Mkinga mkoani Tanga, Emmanuel Mkumbo ambapo ilisema kuwa Mkurugenzi
huyo amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Mororgoro kwa mashtaka sita,
likiwamo la kutishia kuua.
Sasa leo
October 18 2016 taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya
Rais, Ikulu, Gerson Msigwa imesema kwamba Rais Magufuli ametengua uteuzi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga
Emmanuel Mkumbo. Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa uteuzi wa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga atakayejaza nafasi ya Mkumbo
utafanywa baadaye.
Hata hivyo taarifa hiyo ya Ikulu haijaeleza sababu ya utenguzi huo.
No comments:
Post a Comment