Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva, amempa ushauri wa bure
mshambuliaji wake Laudit Mavugo kwa kumtaka kupunguza presha ili aweze
kufanya vizuri uwanjani.
Aveva amesema, Mavugo ni mchezaji mzuri
lakini amekuwa na papara na uchu wa kufunga mabao na anapokosa mambo
humuwia vigumu na kujikuta anashindwa kufanya vizuri awapo uwanjani.
“Tutamtafutia watu wa saikolojia waweze kuongea naye ili aweze kurudi
kwenye kiwango chake, tunachojua yeye ni mchezaji mzuri mwenye uwezo
mkubwa kama atatulia na kufuata maelekezo ya kocha na asisikilize kelele
za mashabiki,” amesema Aveva.
Mavugo alitua kwa mbwebwe kwenye klabu hiyo miezi mitatu iliyopita na
kuonyesha uwezo mkubwa ikiwemo kufunga bao kwenye mechi yake ya kwanza
ya utambulisho wake dhidi ya AFC Leopard ya Kenya na baada ya hapo
alianza kwa kasi mechi za ligi ya Vodacom kwa kufunga mabao matatu
katika mechi zilizoongozana lakini baada ya hapo imekuwa kazi bure
hajafunga bao katika mechi tano zilizopita na amekua akianzishwa benchi
katika mechi mbili za hivi karibuni.
Tuesday, October 18, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment