Gari la misaada lililodaiwa kushambuliwa na Urusi mwezi uliopita |
Urusi imesema imetuma mfumo wa kuzuia makombora katika mji wa bandari wa Tartus nchini Syria. Hatua hiyo inakuja huku hali ya vuta nikuvute kati ya Urusi na Marekani ikipamba moto kuuhusu mzozo wa Syria. Tangazo hilo la Urusi linakuja baada ya Marekani kusema inasitisha mazungumzo na Urusi ya kuyafufua makubaliano ya kusitisha mapigano Syria kutokana na Urusi kuendelea kuunga mkono utawala wa Rais Bashar al Assad.
Majeshi ya Syria yameendeleza mashambulizi makali yanayoulenga mji unaodhibitiwa na waasi wa Aleppo. Urusi imeshutumiwa kwa kufanya mashambulizi ya angani yanayowalenga raia na hospitali katika mji huo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesema ana nia ya kuutafutia ufumbuzi wa kidiplomasia mzozo wa Syria lakini mazungumzo kati yake na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov yamekwisha. Viongozi wa kiusalama na wa sera za kigeni wa Marekani wanakutana leo kujadili njia za kidiplomasia, kijeshi, kijasusi na kiuchumi kuihusu Syria.
No comments:
Post a Comment