MFALME WA THAILAND AFARIKI DUNIA - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Friday, October 14, 2016

MFALME WA THAILAND AFARIKI DUNIA


Mfalme wa Thailand mfalme Bhumibol Adulyadei ambaye ndiye mfalme aliyedumu kwa muda mrefu zaidi amefariki dunia.

Mfalme huyo alienziwa sana nchini Thailand na amekuwa akitazamwa kama nguzo kuu ya kuunganisha taifa hilo ambalo limekumbwa na misukosuko mingi ya kisiasa na mapinduzi ya serikali.
Alikuwa amedhoofika sana kiafya miaka ya karibuni na hajakuwa akionekana hadharani sana.

Kifo chake kimetokea huku Thailand ikisalia chini ya utawala wa kijeshi kufuatia mapinduzi yaliyotekelezwa 2014.

Ikulu ilikuwa awali imeonya kwamba hali yake ya afya ilikuwa imedhoofika zaidi Jumapili.



No comments: