Watu 12 wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia nyumba moja ya malazi mjini Mandera, kaskazini mashariki mwa Kenya.
Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe amesema watu sita wameokolewa kutoka kwenye hoteli hiyo ya Boshari.
Wanamgambo wanaoaminika kuwa wa kundi la al-Shabaab walishambulia nyumba hiyo mwendo wa saa tisa unusu usiku. Walirusha vilipuzi kwenye nyumba hiyo kabla ya kuingia ndani na kuanza kuwafyatulia risasi waliokuwemo ndani.
"Sehemu ya jumba iliporomoka, na kuua watu 12. Watu sita wametolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo hilo wakiwa hai kufikia sasa," ameandika Bw Kiraithe kupitia mtandao wa Twitter.
Wataalamu wa mabomu wanafanya uchunguzi kubaini ni vilipuzi vya aina gani vilitumiwa kutekeleza shambulio hilo.


No comments:
Post a Comment