Bw Trump amekuwa akitafuta uungwaji mkono katika jimbo hilo na ameratibiwa kuwa na mikutano mitano ya kampeni. Bi Clinto pia anaangazia kampeni zake katika jimbo hilo.
Bi Clinton anaongoza kwa alama tatu kwa mujibu wa kura ya maoni ya CBS/YouGov.
Waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje ana 46% ya kura akilinganishwa na mpinzani wake Bw Trump aliye na 43%, kwa mujibu wa kura hiyo ya maoni.
Kura ya maoni ya taifa ya CNN/ORC inaonyesha Bi Clinton yupo alama sita mbele ya mpinzani wake miongoni wa wapiga kura watarajiwa, akiwa na 51% dhidi ya Bw Trump 45%.
Trump: Tuko nyuma lakini hatukati tamaaObama: Trump hafai kuwa rais
Kura za maoni katika ngome za Republican katika majimbo ya Arizona, Georgia na Utah zimeonesha ushindani ni mkali kuliko ilivyotarajiwa.
Lakini akihutubu katika mkutano wa kampeni St Augustine Jumatatu, Bw Trump, alisema: "Jamaa, tunashinda. Tunashinda. Tunashinda."
Kwa mara nyingine amewalaumu wanahabari.
Amewashutumu pia wanaofanya utafiti wa kura za maoni.
Bw Trump amesema barua pepe za John Podesta zilizofichuliwa zinaonyesha mwenyekiti huyo wa kampeni wa Bi Clinton "anatumia udanganyifu kwenye kura za maoni kwa kuhakikisha wafuasi wengi wa Democratic wanashirikishwa".
Umuhimu wa kura zinazopigwa mapemaZaidi ya Wamarekani 6m tayari wamepiga kuraInakadiriwa kwamba 46m watakuwa washapiga kura kufikia siku ya uchaguzi, 40% ya wapiga kura woteKatika jimbo muhimu la Carolina Kaskazini, wapiga kura wafuasi wa Democratic waliojiandikisha kupiga kura wameitisha karatasi za kura za mapema kushinda wenzao wa Republican

No comments:
Post a Comment