Wanadiplomasia wa Afrika kusini wamearifu umoja wa mataifa juu ya uamuzi huo na kuilaumu ICC kwa kuzilenga zaidi nchi za Afrika.
Uamuzi
wa Afrika kusini kujiondoa ulitokana na shinikizo ilikumbana nazo mwaka
uliopita za kuitaka imkamate rais wa Sudan Omar al Bashir wakati wa
mkutano wa muungano wa nchi za Afrika mjini Johannesburg.
Septemba
mwaka jana, mahakama nchini nchini Afrika Kusini iliinyima serikali ya
nchi hiyo ruhusa ya kukata rufaa uamuzi ulioishutumu kwa kukosa
kumkamata Bw Bashir alipohudhuria kongamano hilo mwezi Juni mwaka 2015.
Serikali
ilitaka kukata rufaa uamuzi wa Mahakama Kuu ikisema Bashir alikuwa na
kinga ya urais kwa sababu yeye ni kiongozi wa taifa.
Lakini Jaji Hans Fabricius alisema rufaa hiyo haiwezi kufanikisha chochote.
Aliongeza
kuwa Afrika Kusini ni mwanachama wa Mkataba wa Roma uliounda mahakama
hiyo, na kwamba mkataba huo unabatilisha sheria zozote ambazo huenda
zingempa kinga Bashir asikamatwe na kushtakiwa.
Friday, October 21, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment