EUROPA: POGBA AING'ARISHA MAN UNITED, TIMU YA SAMATHA YAFANYA KWELI. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Friday, October 21, 2016

EUROPA: POGBA AING'ARISHA MAN UNITED, TIMU YA SAMATHA YAFANYA KWELI.

Pogba amefunga magoli mawili katika ushindi wa 4-1 walioupata Man United dhidi ya Fenerbahce.

Pogba mchezaji ghali zaidi duniani alifunga goli la kwanza kwa penalti baada ya Juan Mata kuangushwa ndani ya eneo la hatari, kisha baadaye kuandika bao la pili baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Jesse Lingard.
Goli la Pili kwa United liliwekwa kimiani na Anton Martial kwa njia ya penalti baada ya kuangushwa ndani ya eneo la hatari huku la mwisho likipachikwa na Jesse Lingard kwa shuti kali la chinichini.

Robin Van Persie aliiandikia timu yake ya Fenerbahce goli la kufutia machozi lililoshangiliwa na mashabiki wa pande zote akiwemo kocha wake wa zamani Sir Alex Ferguson.

Katika mechi nyingine timuanaiyoichezea mtanzania Mbwana Samatha ya Genk, imefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Athletic Bilbao kwa magoli ya J.Brabec dk ya 40,na O Ndidi dk.83.

MATOKEO YOTE EUROPA:





No comments: