Mwanasheria wa wilaya katika mji wa Charlotte Steve Kunzweiler amefungua kesi ya mashtaka ya mauaji dhidi ya Afisa Betty Shelby.
Bi Shelby ndiye askari aliyefyatua risasi na kumuuawa Terence Crutcher, 40, mmarekani mweusi wiki iliyopita wakati alipokuwa amesimama karibu na gari lake lilolokuwa limeharibika.
Bi.Shelby alidai Mr Crutcher hawakufuata amri yake alipomuamuru aweke mikono kichwani.
Lakini picha za angani zilizopigwa na helikopta ya polisi zilionyesha Mr Crutcher kutembea mbali na Afisa Shelby na mikono yake ikiwa kichwani kabla ya kujishikilia katika gari lake bila kujaribu kuweka mikono mfukoni kama madai ya Bi.Shelby.
Maswali bila majibu:
Katika video iliyotolewa na polisi haikuonekana kama Bw Crutcher alijaribu kushusha mikono yake.
Familia ya Crutcher ilipinga madai ya Bi Shelby, ikisema kuwa dirisha lake lilifungwa wakati wa tukio hilo.
Polisi wamesema hakuna bunduki iliyopatikana kwa bw. Crutcher wala ndani ya gari lake ingawa madai ya awali yalionesha marehemu huyo kukutwa na silaha.
Chanzo:BBC.COM
No comments:
Post a Comment