BODI YA GAZETI LA UHURU YAJIUZURU - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Friday, September 23, 2016

BODI YA GAZETI LA UHURU YAJIUZURU

Bodi ya Uhuru Media Group inayosimamia vyombo vya habari vya CCM imejiuzulu kupitia barua ya Mwenyekiti wake, Al-haj Adam  Kimbisa.

Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli amepokea barua ya kujiuzulu kwa bodi hiyo leo Septemba 22, 2016 ambayo nakala yake imenakiliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana.

Taarifa ya CCM imesema barua hiyo inaeleza kuwa Kimbisa na wajumbe wote wa Bodi hiyo wameamua kwa hiyari yao kujiuzulu nafasi zao, ikiwa ni siku tatu baada ya Rais Magufuli kutembelea vyombo hivyo na kubaini matatizo katika uendeshaji wake.


No comments: