MAUAJI YA WEUSI YAENDELEA MAREKANI-MAANDAMANO MAKUBWA YATOKEA - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Thursday, September 22, 2016

MAUAJI YA WEUSI YAENDELEA MAREKANI-MAANDAMANO MAKUBWA YATOKEA

Waandamanaji Marekani
Polisi wametumia mabomu ya machozi kuzuia ghasia na  kutawanya umati mkubwa wa watu wenye hasira waliokuwa wamekusanyika katikati ya mji wa Charlotte, nchini Marekani.
Katika ghasia hizo mtu mmoja aliuawa kwa risasi.
Serikali katika eneo hilo imeyaita mauaji hayo kama ya raia kwa raia.
Maandamano na Ghasia zilizuka Jumanne usiku baada ya polisi kumuua Keith Lamont Scott, huku wakisema kwamba kijana huyo alikuwa na bunduki na kwamba alipuuza wito wa kuweka silaha chini.
Hata hivyo familia ya kijana huyo imesema kuwa hakuwa amebeba silaha yoyote
Meya wa mji huo, Jennifer Roberts, ameiambia BBC kuwa aliwataka polisi kumwonyesha mkanda wa video ya tukio hilo.

No comments: