MANCHESTER WAIVURUGA LEICESTER, POGBA ANG'AA ,ROONEY NJE. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Saturday, September 24, 2016

MANCHESTER WAIVURUGA LEICESTER, POGBA ANG'AA ,ROONEY NJE.

 Manchester United imewafunga mabingwa waLigi Kuu Leicester City bila nahodha Wayne Rooney huku mchezaji Paul Pogba akifunga goli lake la kwanza kwa timu hiyo.

Kichwa cha Chris Smalling dk.22 kiliipa uongozi klabu ya Man United akifuatiwa na  Matta aliyefunga goli la pili dk ya 37.

Marcus Rashford aliifungia Manchester goli la tatu baada ya kumalizia pasi iliyopigwa chini kutoka upande wa kushoto.

Paul Pogba aliifungia klabu yake goli la kwanza dk.42 kwa kichwa safi kilichomshinda kipa wa Leicester City.
Goli la Leicester limefungwa na Gray dk. ya 59.


No comments: