HII NDIO TIMU ILIYOFUNGWA 43-0, GOLI KIPA AISHIA POLISI - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Friday, September 23, 2016

HII NDIO TIMU ILIYOFUNGWA 43-0, GOLI KIPA AISHIA POLISI

Ujerumani,
Kivutio au kituko cha mwaka kilikuwa kwenye mchezo wa ligi ndogo ya ridhaa ya Ujerumani ambako hadi dakika 90 matokeo ya mchezo yaligeuka karaha hasa kwa kwa kipa.

Katika michezo huo, klabu ya SV Vonderort ilivunja rekodi ya kufungwa mabao mengi ilipokubali kipigo cha mabao 43-0 dhidi ya mahasimu wao, PSV Oberhausen.

Gazeti la Ujerumnai la Express lilieleza kuwa  SV Vonderort  ilikuwa nyuma kwa mabao 35-0 hadi mapumziko (dakika 45), jambo lililogeuka gumzo.

Badaa ya dakika 45, klabu hiyo iliamua kuingiza  uwanjani wachezaji wanane, lakini wababe wao, PSV Oberhausen kipato kinawapa majivuno zaidi na kuamua kuwatoa wachezaji watatu.

Baada ya kufungwa bao la 36 ndani ya dakika mbili za kwanza za kipindi cha pili, kipa Marco Kwiotek alionekana kama aliyesahau anachofanya uwanjani.

Baada ya mchezo huo, siku tano baadaye katika mazoezi yao, magari mawili za polisi yaliwasili  uwanja wa klabu hiyo, Vonderort uliopo Bottrop, magharibi mwa Dortmund.

Kipa Kwiotek mwenye miaka 25 aliyefungisha mabao hayo mengi alikamatwa na kupelekwa kituoni kwa mahojiano kuhusu tukio la mechi hiyo.

Source: MWANANCHI & THE SUN


No comments: