Shughuli ya kupiga kura inaendelea nchini India, taifa lililo kubwa zaidi duniani linaloongozwa kidemokrasia.
Watu milioni 814 watachagua kati ya chama kinachotawala cha Congress na chama cha Upinzani cha Hindu nationalist BJP .
Uchaguzi
huu utaandaliwa katika mikondo 9 zikianzia majimbo ya Assam na Tripura
zilizoko Kaskazini Mashariki mwa taifa hilo kubwa.
Shughuli
hiyo kubwa zaidi ya Kidemokrasia duniani itachukua majuma matano
kukamilika kutokana na changamoto ya maswala ya mipango usalama na idadi
.
Chama
kinachotawala cha Congress kinakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa
chama cha mrengo wa kulia cha Hindu BJP, kinachoongozwa na Narendra
Hodi, kiongozi mbishi mwenye ushawishi mkubwa kutoka Magharibi mwa
Gujerati.
Kampeni za uchaguzi huo zimetawaliwa na maswala ya ufisadi pamoja na mfumuko wa bei ya bidhaa za Chakula.
Aidha Kuna Chama mahsusi ya Kupambana na Ufisadi yaani AAP (Anti-corruption party).
Chama
hicho kipya kiliwaduwaza wachanganuzi wa maswala ya kisiasa nchini humo
kilipotwaa ushindi muhimu katika Uchaguzi mdogo uliofanyika mji mkuu wa
India New Delhi mwaka uliopita.
Chama hicho sasa kimewakilisha wagombea katika maeneo bunge yote 543
Bunge la
chini la kitaifa ( Lok Sabha) linawajumbe 543 na chama chochote
kinahitaji ushindi wa wajumbe 272 kuunda serikali mpya .
Idadi ya
wapiga kura ni milioni 814 zaidi ya wapiga kura milioni 100 million
zaidi ya wale waliopiga kura katika uchaguzi uliopita wa mwaka wa 2009.
Kutakuwa na vituo 930,000 takriban vituo laki moja zaidi ya vituo vilivyotumika mwaka wa 2009.
Mashini
za kielektroniki za kupigia kura zitatumika na kwa mara ya kwanza
hazitajumuisha kidude cha kutowachagua wawakilishi waliosajiliwa yaani
None of the Above (Nota).
Mwandishi
wa BBC aliyeko katika jimbo la Assam, Sanjoy Majumderameripoti kuwa
wapiga kura walijitokeza kwa wingi asubuhi na mapema wakiwa wamevalia
mavazi ya kitamaduni ya Sari huku wakiwa wamejitanda mitandio ya
Kiassamese.
Wagombea
wakuu ni mwakilishi wa familia ya Nehru-Gandhi, Rahul Gandhi wa chama
cha Congress ambaye atakuwa akipambana dhidi ya Narendra Modi wa chama
kikubwa cha upinzani BJP.
(MM)
No comments:
Post a Comment