TRUMP KIKAANGONI TENA MAREKANI - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Wednesday, May 17, 2017

TRUMP KIKAANGONI TENA MAREKANI


Rais wa Marekani Donald Trump ameteta uamuzi wake wa kujadili taarifa za ndani za marekani juu ya ugaidi na usalama wa ndege na Waziri wa mambo ya ndani wa Urusi, akisema hiyo ni haki yake.

Trump alikuwa na mkutano na waziri wa wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov ambapo aliishirikisha Urusi taarifa zinazoaminika kuwa ni za siri na za kiintelijensia ambazo ingawa hazikuwa kosa kuzitoa lakini wataalamu wa usalama wanaamini hazikupaswa kuvuja nje ya serikali ya Marekani.

Taarifa hizo zilihusu mpango wa kundi la kigaidi la Islamic State(IS) kutumia komputa za Laptop kama silaha katika ndege.

Viongozi wa Republicans na Demokrati wameonesha kukerwa na kitendo hicho huku kiongozi wa demokrati Chuck Schumer akitaka itolewe nakala juu ya mkutano huo.

Kamati ya usalama ya Seneti ya Marekani imeagiza kupatiwa nakala zozote zilizochukuliwa katika mkutano huo.

Licha ya Ikulu ya marekani kukanusha juu ya uharamu wa kutoa taarifa hizo, wataalamu wa mambo ya usalama wamekuwa na wasi wasi juu ya usalama wa maisha ya  vyanzo vya taarifa hizo ambapo kuwekwa wazi kwa taarifa hizo kunahatarisha maisha yao.

Wataalamu wanahofu kuwa kama kuna watu wa kutoka vikundi vya Jihad au wanausalama wa Marekani waliojipenyeza katika makundi ya kigaidi wanaotoa taarifa hizo ni wazi kuwa wapo mahali karibu na makundi hayo ya kigaidi hivyo kutoa taarifa hizo kunawaanika wazi watoa taarifa hao na kuwapa mwanya magaidi kutambua wabaya wao.

Mkurugenzi wa CIA anatarajiwa kuongelea kuhusu mkutano huo huo baadae leo.

No comments: