MAAMUZI YA POLISI BAADA YA ADAM MALIMA KUZOZANA NA ASKARI. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Tuesday, May 16, 2017

MAAMUZI YA POLISI BAADA YA ADAM MALIMA KUZOZANA NA ASKARI.


Jana May 15, 2017 ilisambaa video ikimuonesha aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha kwenye awamu ya nne, Adam Malima akizozana na askari polisi kwa kilichoelezwa kuwa ni baada ya dereva wa kiongozi huyo kupaki gari sehemu isiyotakiwa.
Tukio hilo lilipelekea askari kumtaka dereva wa kiongozi huyo kupeleka gari kwenye Yard ya kampuni moja inayosimamia sheria za barabarani ambapo ilielezwa kuwa dereva alikataa kutii kitendo kilipelekea kuibuka majibizano kati yao.
Leo May 16, 2017 Kiongozi huyo amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka ikiwemo kumzuia askari kutekeleza kazi yake ambapo mtuhumiwa huyo ameachiwa kwa dhamana baada ya kusaini bondi ya Tsh. Milioni 5.

No comments: