Wenyeji Gabon wameanza vibaya mashindano ya soka ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 kwa kipigo cha magoli 5-1 kutoka kwa Guinea katika mchezo wa kwanza wa kundi A.
Guinea Walitawala kabisa kipindi cha kwanza na kuongoza kwa ushindi wa magoli 5-0, kabla ya Gabon kufuta machozi kwa goli moja kipindi cha pili.
Katika mechi nyingine ya kundi A Ghana wameifunga Cameroon magoli 4-0.
MECHI ZA KUNDI B:
Tanzania leo inafungua michezo ya kundi B dhidi ya Mali, huku Niger wanakutana na Angola huko katika mji wa Libreville.
No comments:
Post a Comment