Haya ndiyo mambo muhimu unayopaswa kuyafahamu kuhusu wahombea hawa;
1.Kura ya maoni inaonyesha kuwa Trump anaendelea kupoteza umaarufu wake baada ya kukabiliwa na madai ya kuwanyanyasa kingono wanawake.
2.Bi Clinton bado hana umaarufu mkubwa miongni mwa wapiga kura wa Marekani na amekabiliwa na vichwa vibaya vya habari kuhusu utumizi wa barua pepe za kibinafsi.
Wamarekani wengi watapiga kura Novemba 8.
Mamilioni ya watu wanatarajiwa kuutazama mjadala huo katika chuo kikuu cha Las Vegas ,mjini Nevada,ambao utaongozwa na mwandishi wa habari wa Fox News Chris Wallace.
Wagombea hao watajadili maswala sita ikiwemo deni la kitaifa,afya,faida za kijamii,uhamiaji,uchumi,mahakama ya juu,maswala ya kigeni na hali ya afya yao kuwa rais.

No comments:
Post a Comment