LIGI KUU LEO: YANGA,SIMBA ZAFANYA KWELI, AZAM YAPIGWA. - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Wednesday, October 12, 2016

LIGI KUU LEO: YANGA,SIMBA ZAFANYA KWELI, AZAM YAPIGWA.

Ligi kuu bara leo imeendelea katika viwanja tofauti ambapo imeshuhudia michezo mitano kutoka katika viwanja mbali mbali, katika mchezo wa kwanza timu ya Simba sports club ya jijini Dar es salaam imeinyosha Mbeya City kwa magoli 2-0,magoli ya Simba yakifungwa na Ibrahim Ajib dk.6 na Kichuya dk.ya 36.

Kwaupande wa mahasimu wao Yanga leo walikuwa uwanja wa uhuru ambao ndiyo uwanja wao wa nyumbani wakiwakaribisha walima miwa wa Mtibwa Sugar katika mchezo huo Yanga wamefanikiwa kuibuka na ushindi mwanana wa magoli 3-1,magoli ya Yanga Yakifungwa na Obrey Chilwa dk.45,Simon Msuva, na Donald Ngoma dk.80.Huku lile la Mtibwa likifungwa na Haruna Chanongo dk.64.

Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa leo October 12 2016
  • Mbeya City 0-2 Simba
  • Mbao FC 3-1 Toto Africans
  • Mwadui FC  2-0 African Lyon
  • Majimaji FC 0-1 Kagera Sugar
  • JKT Ruvu 0-0 Prisons
  • Stand United 1-0 Azam FC

No comments: