Rais Magufuli ametinga bandarini hapo jana na kuagiza mkataba kati ya serikali na kampuni ya TICTS kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha serikali inanufaika na mkataba huo.
Katika ziara yake hiyo rais Magufuli alikagua mashine za kukagulia mizigo bandarini hapo ambapo alibaini kuwa ni mashine mbili tu kati ya mashine nne zinazofanya kazi hapo, ambapo mbili ni mbovu na zimesimama.Baada ya hilo rais Magufuli alizipa TPA na wizara ya ujenzi miezi miwili tu kuhakikisha zinanunua mashine mpya ilikuongeza ufanisi.
Pia rais Magufuli alitembelea eneo la mita za kupima mafuta yanayopakuliwa melini na kukuta zote hazifanyi kazi na akaagiza mara moja kununuliwa kwa mita hizo.
No comments:
Post a Comment