KOCHA WA UINGEREZA ABWAGA MANYANGA - ANGA ZA KIMATAIFA

Latest

Wednesday, September 28, 2016

KOCHA WA UINGEREZA ABWAGA MANYANGA

Kocha wa England, Sam Allardyce amejiuzulu nafasi yake ya umeneja kufuatia shutuma nzito za kuonekana kwenye video akitoa ushauri wa jinsi wa kupindisha sheria za usajili za FA kuvuja.


Video hiyo iliyovujishwa na mtandao wa The Daily Telegraph lilichapisha kipande cha video kilichodaiwa kumwonesha Allardyce akiwaambia watu wawili ambao wanahisiwa kuwa ni kutoka Mashariki ya Mbali kwamba angewapa mbinu ya kupindisha sheria za usajili wa wachezaji za FA kwa kutumia njia ya ‘third-party ownership’.

Alladayce alidaiwa kulipwa kiasi cha euro 400,000 ili kukamilisha mpango huo na kufanikisha zoezi zima.

“FA inathibitisha kwamba Sam Allardyce ameacha nafasi yake kama meneja wa England,” taarifa rasmi ya FA imeeleza.

“Kitendo alichokifanya Allardyce, kama ilivyoripotiwa leo, hakikuwa cha kiungwana hasa kwa meneja wa England. Amekubali kwamba amefanya kosa kubwa na tayari ameomba radhi. Hata hivyo kutokana na ukubwa wa shutuma, kwa pamoja FA na Allardyce wameamua kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba mara moja.

“Huu si umamuzi ambao umechukuliwa kijuu-juu isipokuwa baada ya kufikiria kwa kina ili kulinda maslahi mapana ya mchezo wa soka na kuendelea kuufanya mchezo kuendelea kuwa na heshima kubwa.

“Meneja wa timu ya England ya wakubwa lazima adumishe misingi imara ya nidhamu na kuonesha heshima katika mchezo wa soka kwa nyakati zote.

“Gareth Southgate atachukua nafasi hiyo na kusimamia michezo ijayo dhidi ya Malta, Slovenia, Scotland na Uhispania wakati huo FA ikianza mchakato wa kusaka kocha mpya.
“FA inapenda kumtakia Sam kila la heri kwa siku zijazo.”ilisemataarifa hiyo ya FA.

Kocha Gareth Southgate ambaye ni kocha wa kikosi cha chini ya miaka 21 atachukua jukumu la kuinoa timu hiyo kwa muda.

No comments: